Caution: JavaScript execution is disabled in your browser or for this website. You may not be able to answer all questions in this survey. Please, verify your browser parameters.

Utafiti wa iCARE: Utafiti 4

Sisi ni kundi la watafiti wanaozidi 150 kutoka nchi zaidi ya 40. Viongozi wa utafiti huu ni Maprofesa Kim Lavoie, (PhD) na Simon Bacon, (PhD), wakurugenzi wa Montreal Behavioural Medicine Centre (MBMC), Montreal, Canada.

Tungependa kuelewa ufahamu wa umma, mitazamo ya watu, imani za watu, na tabia za watu, kuhusu ugonjwa wa Korona (COVID-19), ambao pia unajulikana kama coronavirus ama virusi vipya vya Korona, ulimwenguni kote. Pia, tunataka kujua jinsi janga hili linavyoathiri nyanja tofauti za maisha ya watu. Ili kutekeleza haya, tunawauliza watu kutoka nchi mbalimbali kukamilisha utafiti huu. Pia, tungependa kupata maoni tofauti tofauti, kwa hivyo mtu yeyote anaweza kukamilisha utafiti huu, bila kujali umri, jinsia, msingi na kule atokako.

Unahitaji dakika ishirini kukamilisha utafiti huu. Hakikisha ya kwamba unaweza kutenga muda wa kutosha, kwa sababu huwezi kujibu maswali kadha, ukaachia njiani halafu urudi baada ya muda fulani kukamilisha. Ukianza kujibu maswali, hakikisha unajibu maswali yote kwa kikao kimoja.

Hatutakusanya habari za kuwatambulisha wale ambao wanashiriki katika utafiti huu, kwa hivyo majibu yako hayatakutambulisha. Uko huru kujiondoa wakati wowote na unaweza kuamua kutojibu maswali yoyote. Hakuna hatari zinazohusiana na kushiriki kwako katika utafiti huu.

Data yote kutokana na utafiti huu itawekwa kwa siri katika seva ya Chuo Kikuu cha Quebec cha Montreal (Canada) kwa miaka 10. Kwa kuheshimu mikataba ya kimataifa ya kueneza data iliyoungwa mkono na Mfuko wa Utafiti wa Quebec (Fonds de la recherche du Québec - FRQ), data kutokana na utafiti huu itaweza kufikiwa na washiriki wote wa utafiti.  Nakala zote za data ya utafiti zitahifadhiwa kwenye seva salama zenye neno la siri ambazo zinaweza kupatikana tu na watu walioruhusiwa.

Matokeo makuu ya utafiti huu yatawekwa hadharani kwenye tovuti (www.mbmc-cmcm.ca/covid19), ambapo kila mtu ataweza kuyasoma.

Ukiwa na swali lolote kuhusu utafiti huu, tafadhali wasiliana na sisi kwa baruapepe ifuatayo: covid19study@mbmc-cmcm.ca.

Utafiti huu umeruhusiwa na shirika la utafiti la CIUSSS-NIM (Centre intégré universitaire de santé et de services sociaux du Nord de l’Île de Montréal: https://www.ciusssnordmtl.ca/). Watafiti wasimamizi, Maprofesa Kim Lavoie na Simon Bacon wamekubali kufuata maagizo yote yaliyoko katika fomu hii.

Wakati unapojibu maswali kwenye utafiti huu, tafadhali kumbuka:

  • Alama nyekundu ya kinyota (*) ambayo inaonekana kando ya maswali inamaanisha maswali hayo lazima yajibiwe. Kama huwezi ama hutaki kujibu swali la lazima, tafadhali bonyeza Sijui/Nimechagua kutojibu ndio uendelee.
  • Ukipata matatizo ya kuonyesha utafiti, tafadhali jaribu kutumia kifaa kingine na/ au kivinjari cha tovuti.

Maelezo kwa washiriki wasiozungumza Kiingereza

Tunatumia jukwaa la programu ya uchunguzi kwa Kiingereza. Utayaona maneno katika Kiingereza, lakini tumetoa tafsiri panapowezekana. Hapa kuna maagizo machache ambayo yatakusaidia kujibu utafiti huu:

  • Unapokamilisha kujibu swali (maswali) kwenye ukurasa, bonyeza kifungo cha blue kilichoandikwa “Next” au “Submit”.
  • Ili kuurejelea ukurasa uliopita, bonyeza kifungo cha blue kilichoandikwa “Previous”
  • Usipojibu swali la lazima, kisanduku kitajitokeza ili kukumbusha. Tafadhali bonyeza kifungo cha blue kilichoandikwa “Close” na ukamilishe kujibu maswali.
  • Tafadhali usibonyeze “Exit and clear survey” iliyo upande wa juu wa kulia wa skrini yako, isipokuwa ukitaka kuacha kujibu maswali ya utafiti. Hautaweza kuuacha kujibu maswali ya utafiti huu halafu uurejelee tena baadaye kuendelea, itabidi uanze tena upya. Ukibonyeza “Exit and clear survey” kimakosa, tafadhali bonyeza kifungo kilichoandikwa “Cancel” kwenye kisanduku ambacho kitajitokeza.

 

Kama unakubali kushiriki katika utafiti huu, bonyeza ”Next”.